Wabunge hao pia wameitaka serikali ya Bahrain kujenga misikiti yote ya Waislamu wa madhehebu ya Shia iliyobomolewa na serikali.
Wabunge hao wamesema kuwa uuzaji wa silaha kwa serikali ya Bahrain unapaswa kusimamishwa hadi pale serikali ya Manama itakapowakamata na kuwafikisha mahakamani maafisa waliohusika kuwatesa na kuwaua raia wanaoandamana dhidi ya utawala wa kifalme wa nchi hiyo.
Vilevile wabunge hao wa Marekani wamesisitiza kuwa mwenendo wa kesi za watu wanaotiwa nguvuni unapaswa kufanyika kwa uwazi na maafisa wanaowatesa mahabusu watangazwe kwa wananchi.
Wabunge hao wa chama cha Democrat wametaka kusimamishwa biashara ya silaha na utawala wa Bahrain katika hali ambayo vongozi wa sasa wa Washington wanaitaja Bahrain kuwa ni mshirika wao wa kistratijia na siku zote wamekuwa wakiwaunga mkono watawala hao katika ukandamizaji wao dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia. 875460