Sherehe za kuadhimisha siku ya kuzaliwa Imam Ridha (as) ambaye ni Imam wa Nane wa Waislamu wa madhehebu ya Shia na mmoja wa Watu wa Nyumba ya Mtume (as) zilifanyika Jumamosi iliyopita katika Kituo cha Kiislamu cha Imam Ridha (as) huko Vienna mji mkuu wa Austria.