IQNA

Hizbullah yaunga mkono kikamilifu suala la Palestina

8:35 - October 10, 2011
Habari ID: 2201942
Mkuu wa Kundi la al-Wafau Lilislamu, linalofungamana na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza katika mazungumzo na ujumbe wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas kwamba Hizbullah itaendela kuunga mkono harakati hiyo ya Palestina dhidi ya adui wa Uislamu, ambao ni utawala haramu wa Israel.
Muhammad Rad ambaye pia ni kiongozi wa chama cha Hizbullah katika bunge la Lebanon alionana na ujumbe huo uliongozwa na Mahmoud az-Zahhar, mwanachama wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas pamoja na Raf’at Marra, Mkuu wa ofisi hiyo katika eneo la Beirut, mji mkuu wa Lebanon, ambapo walijadili masuala mbalimbali yanayohusiana na matukio ya hivi karibuni kabisa huko Palestina na eneo zima la Mashariki ya Kati.
Viongozi hao hasa walijadili kwa kina masuala yanayohusiana na kambi za wakimbizi wa Kipalestina nchini Lebanon, mapatano ya maelewano ya makundi ya Palestina ya Hamas na Fat’h na mzingiro unaotekelezwa na Wazayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza.
Pande mbili hizo zilisisitiza katika mazungumzo yao kwamba wakimbizi wa Palestina wanaoishi nje ya nchi hiyo inayokaliwa kwa mabavu na utawala wa Israel kamwe hawataisahau nchi yao kwa sababu inafungamana moja kwa moja na akili pamoja na dhamira zao. 876023
captcha