Watawala wa utawala huo wametoa amri ya kubomelewa sehemu ya msikiti huo kwa kisingizio kuwa ulijengwa bila kibali cha serikali, katika hali ambayo ni siku chache tu zimepita tokea walowezi wa Kizayuni wavunjie heshima makaburi ya Waislamu na Wakristo katika mji huo.
Watawala hao wanasema wamechukua hatua ya kubomoa sehemu moja ya msikiti huo kutokana na kuwa iliongezwa kwenye msikiti mkuu bila ruhusa ya serikali.
Utawala haramu wa Israel umetoa muda wa miezi miwili kwa Waislamu wa mji huo wawe wamebomoa sehemu hiyo mpya la sivyo watawaamuru maafisa wa halmashauri ya mji huo kuibomoa. 876907