IQNA

Operesheni za kujitolea kufa shahidi, kujibu mashambulio dhidi ya Lebanon

16:37 - October 11, 2011
Habari ID: 2202897
Akizungumza hivi karibuni na wanachama wa Msafara wa Maryam II, ambao ni msafara unaojumuisha wanawake 151 wa Lebanon ambao wamesafiri katika mji wa Halab nchini Syria kwa madhumuni ya kuonyesha umoja na mshikamano wa nchi mbili hizo jirani, Mufti wa Syria amesema kuwa maadui wa nchi mbili hizo watakabiliwa na operesheni za kujitolea kufa shahidi iwapo watachukua hatua yoyote ya kipumbavu ya kushambulia ardhi za nchi hizo.
Mufti Ahmad Badrudiin Hassun amesema kuwa kwa hakika nchi mbili za Syria na Lebanon ni taifa moja na kwamba kwa msingi huo nchi za Magharibi ambazo zina nia ya kutekeleza njama ya kiuadui dhidi ya mojawapo ya nchi hizo, zinapasa kutambua kwamba wananchi wa nchi hizo wamesimama imara kwa ajili ya kujitolea kufa shahidi katika kulinda ardhi yao.
Mufti wa Syria amesema ukweli huo ulidhihiri wazi katika mashambulio ya kinyama yaliyofanywa na utawala haramu wa Israel mwaka 2006 kusini mwa Lebanon. Amesema licha ya kuwa uchokozi huo wa utawala haramu wa Israel uliacha uharibifu mkubwa katika eneo hilo lakini wananchi wa nchi hiyo na hata Syria wana moyo thabiti wa kuendelea kutekeleza operesheni mbalimbali zikiwemo za kujitolewa kufa shahidi ili kulinda ardhi yao.
Msafara huo pia ulimpa pole Mufti huyo wa Syria kutokana na kumpoteza mwanawe Sariya Ahmad Badrudiin Hassun, katika tukio la kigaidi lililotekelezwa dhidi yake na vibaraka wa Kizayuni. 877564
captcha