IQNA

Machafuko ya Cairo yanatokana na njama za Marekani dhidi ya Waislamu

16:19 - October 11, 2011
Habari ID: 2202898
Harakati ya Mapambao ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah, hapo jana Jumatatu ilitoa taarifa ikielezea wasiwasi wake mkubwa kuhusiana na kuongezeka machafuko kati ya Wakristo na Waislamu wa nMisri na kuongeza kuwa ghasia hizo zinatokana na njama za Marekani dhidi ya Waislamu.
Hizbullah imesema katika taarifa hiyo kwamba ghasia hizo ambazo zinalenga kuwatenganisha Wakristo wa Kikopti na Waislamu wa Misri bila shaka ni njama za maadui wa Waarabu, Wakristo na Waislamu na zinazokusudia kuvuruga usalama wa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika kwa manufaa ya Marekani na utawala haramu wa Israel.
Taarifa hiyo imesema ghasia hizo ambazo zimepelekea kuuawa na kujeruhiwa Wamisri kadhaa bila shaka zina lengo la kuigawa nchi hiyo ya Kiislamu katika misingi ya kidini, kimadhehebu na kikabila.
Hizbullah imewataka Wamisri wote kuwa macho dhidi ya njama za maadui na kuchagua mazungumzo kama njia bora ya kutatua matatizo yao. 877574
captcha