IQNA

Wazayuni wabomoa msikiti mwingine Palestina

20:59 - October 11, 2011
Habari ID: 2203271
Utawala haramu wa Israel umebomoa Msikiti mwingine katika kitongoji cha Khirbet Yazra kilichoko karibu na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, katika hatua nyingine ya wazayuni ya kuvunjia heshima matukufu ya dini ya Kiislamu.
Gazeti la Palestine Tribune limeripoti kuwa, zaidi ya askari 5 wa jeshi la utawala ghasibu wa Israel wametumia buldoza la kijeshi kubomoa msikiti huo.
Huu ni msikiti wa tatu kubomolewa na askari wa kizayuni katika miezi ya hivi karibuni katika eneo la bonde la Jordan.
Bomoabomoa hiyo ya miskiti ya Waislamu inafnyika sambamba na hujuma zinazofanywa na walowezi wa Kiyahudi dhidi ya Wapalestina madhulumu na ardhi zao.
Wakati huo huo utawala ghasibu wa Israel unaendeleza ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi za Wapalestina zinazokaliwa kwa mabavu, licha ya jamii ya kimataifa kuutaka ukomeshe ujenzi huo haramu mara moja. 877871
captcha