Mwendesha Mashtaka wa serikali ya Tunisia amesema uamuzi huo wa kufungua mashtaka dhidi ya televisheni ya Nasma kwa sababu ya kurusha hewani filamu inayopiga vita Uislamu na Iran ya Persepolis umechukuliwa baada ya malalamiko yaliyowasilishwa na mawakili na raia wa kawaida.
Waislamu na baadhi ya vyama vya siasa vya Tunisia vimewakosoa vikali viongozi wa kanali ya televisheni ya Nasma kwa kurusha hewani fulamu hiyo inayokwenda kinyume na mafundisho ya Uislamu na kusema kuwa kufanyika kitendo hicho tena katika kipindi hiki cha kukaribia uchaguzi kuna malengo makhsusi na kunataka kuzusha fitina.
Sehemu moja ya filamu hiyo ya Persepolis inaonyesha kile ilichodai kuwa ni picha ya Mwenyezi Mungu. 878033