IQNA

Suala la wafungwa, kipaumbele cha serikali ya Palestina

14:24 - October 12, 2011
Habari ID: 2203758
Ismail Hania, Waziri Mkuu wa Palestina amesema kuwa suala la wafungwa na mateka wa Palestina wanaozuiliwa katika jela za kuogofya za utawala haramu wa Isreal ni kipaumbele muhimu kinachozingatiwa na serikali ya Palestina.
Akizungumza hapo jana Jumanne mara tu baada ya kumalizika kikao cha baraza lake la mawaziri, Hania amewashukuru Wapalestina kwa kuunga mkono suala la kuachiliwa huru wafungwa wa taifa hilo. Amewataka pia waendelee kutoa mashinikizo dhidi ya utawala ghasibu wa Israel ili usimamishe mara moja hatua zake za uchokozi na ugaidi dhidi ya Wapalestina wasio na hatia.
Amesema Wapalestina wanajivunia mashujaa wao wanaokandamizwa katika jela za Wazayuni na kwamba kamwe hawatawasahau.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, jana usiku mkuu wa Ofisi ya Masuala ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas pia alisema kuwa kuna uwezekano wa kufunguliwa wafungwa na mateka wote wa kike wa Palestina katika mabadilishano na Gilad Shalit, mateka wa Kizayuni anayeshikiliwa na Hamas.
Akifafanua suala hilo, Khalid Mash'al amesema kuwa mabadilishano hayo yanatazamiwa kufanyika katika hatua mbili, ya kwanza itaanza wiki hii kwa kuachiliwa huru wafungwa 450 wa Palestina. Amesema wafungwa wote wa kike wataachiliwa katika hatua ya pili. Ameongeza kuwa wafungwa hao wanatoka katika pembe zote za Palestina. 878355
captcha