IQNA

Mwanazuoni wa Kishia auawa kigaidi mjini Karbala

14:37 - October 13, 2011
Habari ID: 2204181
Mahand Mi'mar au kwa jina jingine Abu Zeinab, mmoja wa wanazuoni mashuhuri wa Kishia katika mji mtakatifu wa Karbala alilengwa na kuuawa na magaidi hapo siku ya Jumanne usiku.
Mwanazuoni huyo aliuawa katika eneo la Shuhadau Seif Sad mashariki mwa mji huo mtakatifu.
Mwanzuoni huyo aliuawa kwa kupigwa risasi na magaidi waliokuwa kwenye gari moja lililomkaribia alipokuwa akirejea nyumbani kwake mara tu baada ya kuswali swala za Magharib na Ishaa. Aliuawa pamoja na dereva wake binafsi.
Mara tu baada ya kuuawa, polisi usalama walifika mahala hapo kwa haraka na kuanzisha uchunguzi katika tukio hilo la kigaidi.
Tunakumbusha hapa kuwa kwa muda wa miezi kadhaa sasa mji mtakatifu wa Karbalaa umekuwa ukishuhudia vitendo vingi vya ugaidi dhidi ya wanazuoni na raia wasio na hatia wa Kishia, ambapo watu 22 waliuawa shahidi na wengine wengi kujeruhiwa katika tukio la kigaidi lililotekelezwa na magaidi mnamo tarehe Pili Septemba dhidi ya msafara wa Wairaki waliokuwa wakielekea Syria kwa ajili ya kufanya ziara katika maeneo matakatifu nchini humo. 878409
captcha