IQNA

Netanyahu ataka kuhalalisha kisheria ujenzi wa vitongoji

14:41 - October 13, 2011
Habari ID: 2204182
Ikiwa ni katika juhudi zake za kichokozi za kupora ardhi za Wapalestina, Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel ameazimia kubuni kamati itakayofuatilia na kuhalalisha kisheria ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi hizo unazozikalia kwa mabavu.
Kwa mujibu wa gazeti la Intiqad linalochapishwa Lebanon, Netanyahu amesema kuwa atabuni kamati hiyo hivi karibuni kwa madhumuni ya kuchunguza njia za kuhalalisha kisheria ujenzi wa vitongoji katika ardhi za Wapalestina.
Tayari Ya'qub Nu'man Waziri wa Sheria wa utawala huo amepewa jukumu la kutafuta wanachama wa kamati hiyo na kuipa jukumu la kutekeleza masuala yatakayopitishwa na serikali ya Netanyahu katika uwanja huo.
Wakati huohuo Bani Beigan, Waziri Mshauri wa Israel ametangaza kuwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi utaendelea kwa kasi na kwamba hautasimamishwa kwa kisingizio chochote kile cha eti kuanzisha tena mazungumzo na Wapalestina.
Amesema kuwa siasa za utawala huo zimesimama katika msingi wa kubomoa nyumba za Wapalestina kwa ajili ya kuimarishwa ujenzi wa vitongoji hivyo. 878414
captcha