Akifafanua suala hilo, Sheikh Fallah al-Malla kiongozi wa kabila la Bufahd amesisitiza kwamba Wairaki hawana haja kuwa na wakufunzi wa kijeshi wa Marekani nchini humo. Amesema askari wa Marekani wamekuwa Iraq kwa kipindi cha miaka minane iliyopita na kwamba kama wangekuwa na nia, wangekuwa wamekwishatoa mafunzo ya kutosha kwa askari jeshi wa Marekani bila ya kuomba muda wa ziada kwa ajili ya kutekeleza jukumu hilo.
Wakati huohuo, Sheikh Hamid al-Hais, Mkuu wa Baraza la Wokovu la Mkoa wa Anbar amesema Iraq haina haja yoyote ya kupata mafunzo ya kijeshi ya Wamarekani kwa sababu jambo hilo litaimarisha tu uvamizi wa nchi hiyo nchini Iraq bila ya kuwepo faida yoyote ya maana kwa maslahi ya kitaifa. 879795