IQNA

Hamas yalaani ujenzi wa vitongoji vya Mayahudi huko Quds

18:05 - October 15, 2011
Habari ID: 2205228
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imepinga na kulaani vikali uamuzi wa utawala haramu wa Israel wa kujenga nyumba mpya 2600 za walowezi wa Kizayuni katika eneo la Jufaat Hamtus huko kusini mwa Quds Tukufu katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo.
Hamas imetoa taarifa ikisema kuwa hatua hiyo ya kichokozi imelenga kuitenga Quds Tukufu na eneo la Kiarabu la Beit Laham.
Sehemu nyingine ya taarifa hiyo inamtaka Mahmoud Abbas, Mkuu wa Utawala wa Ndani wa Palestina ajiepushe kurejea kwenye meza ya mazungumzo ya mapatano na utawala haramu wa Israel na badala yake ajishughulishe na suala la kuleta umoja wa kitaifa nchini Palestina kama njia ya kutoa radiamali kwa vitendo hivyo vya kujipanua vya Wazayuni katika ardhi za Wapalestina.
Hamas imewataka Wapalestina wote kuwa na umoja na mshikamano kwa ajili ya kupambana na uchokozi zaidi wa utawala wa Kizayuni. 879844
captcha