Shalqam ameiambia kanali ya Televisheni ya al Arabiya kwamba kwa mujibu wa ripoti alizopokea, Imam Sadr aliuawa nchini Libya.
Kuhusu sababu za kuuliwa kwake, Shalqam amesema: "Imam Mussa Sadr alikosoa vikali mitazamo ya Kanali Muammar Gaddafi kuhusu dini ya Kiislamu, suala ambalo lilimkasirisha mno dikteta huyo na kumkamata na kisha kumpeleka kusikojulikana akiwa pamoja na wenzake. Imam Mussa Sadr alikuwa kiongozi wa ngazi za juu wa kidini wa Lebanon.
Kwa mujibu wa matamshi ya waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Libya, Gaddafi alikuwa akiamini kwamba Uislamu unapasa kufanyiwa marekebisho na kwamba maneno kama "قُل" katika aya za Qur'ani yanapaswa kuondolewa.
Abdur Rahman Shalqam alikuwa mwakilishi wa Libya katika Umoja wa Mataifa. Alijiuzulu wadhifa huo na kujiunga na wanamapinduzi baada ya kushadidi ukandamiza wa Muammar Gaddafi dhidi ya waandamanaji. 880175