Sheikh Naeem Qasim alisema jana katika kikao kilichofanyika kwenye ubalozi wa Iran mjini Beirut kwamba tuhuma hizo za Marekani zinashabihiana zaidi na filamu za kipolisi ambazo watengenezaji wake wamefeli katika maisha halisi.
Sheikh Naeem Qasim ameongeza kuwa Marekani imetoa tuhuma hizo za uongo dhidi ya Iran kwa sababu Tehran ndio kikwazo kikuu cha mipango na njama za nchi hiyo katika Mashariki ya Kati.
Amesema moja ya malengo ya tuhuma hizo za uongo ni kuzusha fitina kati ya Waislamu na kufunukia kushindwa kwa siasa za Washington katika Mashariki ya Kati.
Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema katika kipindi chote cha miaka 32 iliyopita Iran imestahamili vikwazo, mashinikizo na njama za aina mbalimbali za adui na kufanikiwa kuvishinda vyote. 880496