Saudi Arabia ilitangaza jana kwamba, kwa ajili ya kulinda amani na usalama wa mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu, hakuna ruhusa ya kufanya kitendo chochote kinachoweza kuzusha fujo katika siku za ibada ya hija ya mwaka huu!
Amir wa eneo la Makka Khalid Faisal amewaambia waandishi habari kwamba serikali haitaruhusu mtu yeyote kufanya tendo litakalohatarisha amani ya mahujaji.
Amir wa Makka amesema kuwa hadi sasa zaidi ya mahujai nusu milioni wamekwishawasili nchini Saudi Arabia na kwamba juhudi zinafanyika kwa shabaha ya kuboresha huduma kwa mahujaji hao. 880725