IQNA

Kituo cha Mazungumzo ya Kidini cha Saudia chakabiliwa na utata Austria

16:38 - October 16, 2011
Habari ID: 2205986
Kituo cha Mazungumzo ya Kidini cha Austria kimekabiliwa na utata mkubwa kufuatia upinzani wa wanasiasa wa nchi hiyo dhidi ya kufunguliwa kwake nchini humo kwa udhamini wa Saudia Arabia.
Saudi Arabia ilitiliana saini na nchi hiyo pamoja na Hispania mkataba wa ujenzi wa kituo hicho mjini Vienna Austria katika hali ambayo wanasiasa wengi wa nchi hiyo wanapinga vikali jambo hilo, kwa hoja kwamba kituo hicho hakitakuwa na faida nyingine isipokuwa kuiarifisha Saudia nchini humo kama nchi inayoheshimu haki za binadamu katika hali ambayo ukweli wa mambo ni kinyume kabisa.
Wanasiasa hao wakiwemo wabunge wa Chama cha Kijani, wanasema kuwa Saudia inapinga uhuru wa kuabudu kwa wafuasi wa dini nyinginezo zisizo za Kiislamu na kwa hivyo haipasi kupewa fursa ya kuonyesha kinyume cha ukweli huo kupitia uzinduzi wa kituo hicho mjini Vienna.
Akizungumzia suala hilo, Omar al-Bayati, Msemaji wa Waislamu Waliberali wa Austria ametahadharisha dhidi ya kuanzishwa kituo hicho kwa hoja kwamba Saudia inataka kukitumia kama njia ya kueneza Uwahabi barani Ulaya, jambo ambalo amesema ni hatari kubwa kwa usalama wa bara hilo.
Kabla ya hapo Ahmad at-Tayyib, Sheikh wa al-Azhar alikosoa uzinduliwaji wa kituo hicho cha Saudia nchini Austria na kusema kuwa kitaharibu zaidi mambo kwa kueneza Uwahabi duniani. 880786
captcha