IQNA

Mayahudi wenye misimamo mikali washambulia tena Masjidul Aqsa

16:28 - October 17, 2011
Habari ID: 2206647
Kundi moja la Mayahudi wenye misimamo ya kupindukia mipaka jana asubuhi kwa mara nyingine tena lilishambulia Msikiti wa al-Aqsa kwa usaidizi wa polisi wa utawala haramu wa Israel.
Watu walioshuhudia tukio hilo wanasema kuwa Mayahudi hao walijaribu kuvuruga ibada za Waislamu waliokuwa wakiswali kwenye msikiti huo mtakatifu na kutishia usalama wao.
Askari walioandamana na Mayahudi hao walisimama kwenye milango ya kuingia kwenye msikiti huo na kuwazua Waislamu na hasa vijana waliokuwa wakielekea huko kuswali.
Mayahudi walio na misimamo ya kupindukia mipaka waliingia kwenye msikiti huo kwa kisingizio cha kutekeleza ibada katika hali ambayo wakazi wa Quds Tukufu walikuwa wamekusanyika humo kwa madhumuni ya kutetea matukufu yao. 881064
captcha