Huku ikitoa taarifa ya kuwaunga mkono wafungwa wa masuala ya kiitikadi wa Azarbaijan, jamii ya Waislamu wa Kishia wa Moscow imesema katika taarifa hiyo kwamba kughafilika na masuala ya kimaanawi ndicho chanzo kikuu cha kuanguka watawala duniani.
Kufuatia kitendo cha serikali ya Baku cha kuwatia nguvuni na kuwafunga jela Washia ambao ndio wanaounda idadi kubwa ya Waislamu wa nchi hiyo, jamii hiyo ya Waislamu wa Moscow imelaani vikali kitendo hicho na kutaka waachiliwe huru mara moja.
Waislamu hao walihukumiwa vifungo vya jela kwa kutetea itikadi na thamani zao za kidini ikiwa ni pamoja na suala la vazi la hijabu na kuimarishwa shughuli za Waislamu misikitini. Wamesema kuwa kuna baadhi ya watu katika serikali ya Azarbaijan ambao wanataka kugonganisha serikali hiyo na Waislamu kwa kukandamiza na kukanyaga haki zao za kidini.
Waislamu wa Moscow wameitaka serikali ya Baku kusimamisha mara moja ukandamizaji huo dhidi ya Waislamu la sivyo watajisababishia matatizo ambayo itakuwa vigumu kwao kuyatatua. 881278