Munawwar Hassan amesema katika hotuba aliyotoa kwenye Chuo Kikuu cha Punjab katika mji wa Lahore kwamba maandamano yanayofanywa na maelfu ya watu barani Ulaya na Marekani yameonyesha kwamba hawana tena imani na mfumo wa ubepari.
Amesema kuwa huko nyuma tulishuhudia kushindwa mifumo ya kikomunisti na kisoshalisti na sasa wananchi wa huko Magharibi wanatangaza kutokuwa na imani tena na mfumo wa kibepari.
Kiongozi wa kundi la Jamaat Islamiya la Pakistan amesema kuwa mfumo wa Kiislamu ndio unaoweza kumuondoa mwanadamu katika minyororo ya kuwa mtumwa wa mwanadamu mwenzake na kumuelekeza kwa Mwenyezi Mungu. 881412