IQNA

Tovuti 10,000 zaupiga vita Uislamu duniani

14:24 - October 18, 2011
Habari ID: 2207217
Imam wa Masjidul Haram mjini Makka, ambaye nchi yake ni moja ya waungaji mkono wakubwa wa makundi yenye mielekeo ya kupindukia mipaka kuhusiana na fikra za Kiislamu, makundi ambayo yamekuwa katika mstari wa mbele wa kukufurisha Waislamu wenzao, amezungumzia suala la kuwepo tovuti 10,000 zinazopiga vita na kuuvunjia heshima Uislamu, na kuyasihi makundi ya Kiwahabi kuanzisha tovuti zaidi katika uwanja huo.
Abdulrahman as-Sudeisi Imam na Khatibu wa Masjidul Haram amezungumzia umuhimu wa kuanzishwa tovuti zaidi za Kiwahabi kwa madhumuni ya kupambana na tovuti alizosema zinapiga vita Uislamu katika hali ambayo fikra za kundi hilo la Kiwahabi zenyewe zinaharibu na kupotosha mafundisho halisi ya dini ya Kiislamu.
Amesema tovuti hizo zinaharibu jina la Uislamu na kwamba Waislamu wanapasa kufanya kila wawezalo ili kukabiliana na hali hiyo.
As Sudeisi amesema gharama inayotumika kuendesha tovuti hizo inapindukia dola milioni moja katika hali ambayo tovuti 200 zinazolenga kuhudumia Uislamu zinaendeshwa kwa kutegemea msaada wa watu wanaojitolea, ambao hawawezi kutegemewa sana katika kudumisha shughuli za tovuti hizo za Kiislamu.
Tunakumbusha hapa kuwa hivi karibuni Kamati ya Kimataifa ya Uhuru wa Kidini, ilitoa taarifa ikisema kuwa utawala wa Saudi Arabia unabana na kutoruhusu makundi mengine ya kidini na kimadhehebu yanayopinga fikra za Kiwahabi, kuendesha shughuli zao nchini humo. 881444
captcha