Salim Miftah al Rafadi amesisitiza kuwa kikosi chake kimegundua maficho ya dikteta Gaddafi katika mji alikozaliwa wa Sirte. Amesema dikteta huyo atatiwa nguvuni hivi karibuni na kwamba kubakia kwake huru ni hatari kubwa kwa amani na usalama wa Libya.
Awali makamanda wa Baraza la Taifa la Mpito la Libya walikuwa wametangaza kuwa Gaddafi amejifisha katika eneo la jangwani la kusini magharibi mwa Libya karibu na mji wa Gaddamis.
Kamanda al Rafadi amesema wanamapinduzi wa Libya wanauzingira mji wa Sirte kutokea pande zote na kwamba hakuna uwezekano wa Muammar Gaddafi kutoroka mji huo. 882531