Maonyesho hayo ambayo yatafanyika chini ya anwani "Mtume Muhammad (saw), Rehema kwa Walimwengu' yameandaliwa na Muungano wa Jumuiya za Kiislamu za Ufaransa na vikao mbalimbali vya kitaalamu vitaandaliwa katika maonyesho hayo ili kuarifisha shakhsia na maisha ya Mtume Mtukufu (saw).
Mazungumzo kati ya wanazuoni mashuhuri wa Ufaransa na wanazuoni kutoka nchi nyingne za Ulaya, maonyesho ya filamu na vitabu vya Kiislamu, picha za maeneo matakatifu ya Kiislamu, mashindano ya hifdhi na kiraa ya Qur'ani Tukufu maalumu kwa vijana pamoja na mashairi ya kumsifu Mtume (saw) ni sehemu ya ratiba zitakazotekelezwa kwenye maonyesho hayo.
Waandaaji wa maonyesho hayo wamewataka Waislamu na wasio Waislamu kuyatembelea ili wapate kufahamu sura halisi ya Uislamu. 882892