IQNA

Maandamano dhidi ya ubepari yaendelea katika nchi za Ulaya

14:30 - October 19, 2011
Habari ID: 2208062
Wapinzani wa mfumo wa ubepari katika nchi za Marekani na Ulaya wameapa kudumisha maandamano hayo hadi matakwa yao yatakapotekelezwa.
Waandamanaji katika nchi za Ulaya na hasa Uingereza, Ujerumani, Hispania na Italia wamekuwa wakifanya maandamano makubwa katika miji muhimu ya nchi hiyo kupinga na kulalamikia sera za ubepari zinazotawala katika nchi za Magharibi.
Jumamosi iliyopita ulimwengu ulishuhudia maandamano makubwa yakifanyika katika nchi 80 muhimu za dunia kupinga mfumo wa ubepari, maandamano ambayo yaligeukana na kuwa ya ghasia katika baadhi ya nchi hizo.
Licha ya polisi ya Marekani kutumia nguvu dhidi ya wapinzani wa mfumo huo katika eneo la Wall Street lakini waandamanaji wameazimia kuendeleza maandamano hayo ambayo sasa yameingia katika mwezi wake wa pili.
Utumiaji nguvu mwingine kama huo ulionekana huko Rome mji mkuu wa Italia hapo siku ya Jumamosi ambapo polisi wa kuzuia ghasia walitumia nguvu za ziada dhidi ya waandamanaji waliokuwa wakiandamana kwa amani kutetea haki zao. 882584
captcha