Sayyid Muhammad Ashraf Kachochawi amesema hayo katika kikao cha wanachama wa baraza hilo na kutoa wito wa kubana uingiliaji wa Saudi Arabia katika masuala ya Waislamu wa India.
Amesema Waislamu wa India wanapaswa kukataa itikadi za Kiwahabi zinazochafua jina na sura ya Uislamu.
Sayyid Muhammad Kachochawi amesema kuwa Waislamu wa India waliwafukuza Mawahabi nchini humo miaka mia moja iliyopita na kwamba baada ya uhuru wa India Mawahabi walianza kueneza tena satua na ushawishi wao nchini humo kutokana na fedha za utajiri wa mafuta ya Saudi Arabia.
Ameongeza kuwa Mawahabi wana ushawishi katika taasisi nyingi za Kiislamu na magazeti na wanafanya jitihada za kuwa na nguvu ya kisiasa nchini India.
Katibu Mkuu wa Baraza la Maulamaa na Masheikh wa India pia ametaka kufanyika uchunguzi na udhibiti wa fedha za shule na madrasa za nchi hiyo ili kuhakikisha kwamba fedha za mafuta za Mawahabi wa Saudia haziingizwi katika shule hizo. 883020