Katibu wa Baraza la Kipapa na msimamizi wa mazungumzo hayo Pier Luigi Celata amesema Sheikh Ahmad Tayyib wa al Azhar hatashiriki katika mkutano huo utakaofanyika tarehe 27 Oktoba.
Amesema kuwa uhusiano wa Vatican na al Azhar ulikatwa mwaka jana kufuatia matamshi yaliyotolewa na Papa Penedict wa 16 kuhusu hali ya Wakristo katika baadhi ya nchi za Kiislamu na kwa sababu hiyo Ahmad Tayyib amesema kuwa hatashiriki katika mkutano wa mazungumzo kati ya dini mbalimbali utakaofanyika Italia ukisimamiwa na viongozi wa Vatican.
Pier Luigi Celata amesema kuwa nchi 19 za Kiislamu zimetangaza kuwa zitashiriki katika mkutano huo. 882999