Huku mahujaji wakizidi kumiminika katika mji mtakatifu wa Makka kwa ajili ya ibada ya hija, Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Saudi Arabia imetangaza kwamba itakuwa ikijibu maswali ya kidini ya mahujai kupitia mtandao wa www.al-islam.com.
Wizara hiyo imesema kuwa imeamua kujibu maswali ya mahujaji kwa njia hiyo ili kurahisisha mawasiliano baina yao na wizara hiyo na pia kujibu kirahisi maswali yao ya kidini.
Akifafanua ziadi suala hilo, Musaid bin Ibrahim al-Hadithi, msimamizi wa masuala ya uchapishaji na utafiti katika wizara hiyo amesema kwamba tovuti hiyo itakuwa na uwezo wa kujibu maswali 200 kwa siku. Amesema kamati maalumu ya wanazuoni na wataalamu wa masuala ya kidini imebuniwa ili kujibu maswali ya mahujaji kupitia tovuti hiyo.
Maafisa wanaohudumu katika kamati hiyo wanatabiri kwamba watafanikiwa kujibu maswali 4000 ya mahujaji ifikapo mwishoni mwa msimu huu wa hija.
Mbinu hiyo ya kujibu maswali ya mahujaji ilianzishwa miaka mitatu iliyopita. 883030