IQNA

Ujumbe wa Hizbullah wawasili mjini Moscow

12:53 - October 20, 2011
Habari ID: 2208409
Ujumbe wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah uliwasili mjini Moscow Russia Jumatano alfajiri kujibu mwaliko wa nchi hiyo.
Ujumbe huo unawajumuisha Muhammad Rad, mkuu wa kundi linalofungamana na Hizbullah la Utiifu kwa Mapambano katika Bunge la Lebanon, Hassan Fadhlullah, Mkuu wa Kamati ya Maelezo na Mawasiliano ya Bunge la Lebanon na Nawar as-Sahili mbunge mwingine mashuhuri wa Lebanon.
Ujumbe huo umekutana na wakuu wa Duma, bunge la Russia, Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo na vilevile maafisa wanaoshughulikia masuala ya kidini katika kitengo cha bara Ulaya.
Safari ya ujumbe huo nchini Russia ina umuhimu mkubwa kwa kutilia maanani matukio yanayoendelea sasa duniani na hasa katika nchi za Kiarabu za Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika.
Kufafanuliwa viongozi wa Russia matukio halisi ya Lebanon mbali na misimamo ya baadhi ya nchi za Ulaya zinazotaka kuichafulia jina Hizbullah ni moja ya malengo muhimu ya safari hiyo. 883113
captcha