IQNA

Wanamapinduzi wa Libya wataka familia ya Gaddafi irejeshwe nchini humo

16:31 - October 22, 2011
Habari ID: 2209385
Mahmoud Jibril, Mkuu wa Kamati Andamizi ya Baraza la Mpito la Kitaifa la Libya ameitaka Algeria kurejesha nchini humo familia ya dikteta Muammar Gaddafi.
Amesema, kutokana na kuwa Gaddafi ameuawa na wanamapinduzi, na hivyo kuanza awamu mpya ya historia ya Libya, familia ya dikteta huyo wa zamani inapasa kurejeshwa nchini humo mara moja.
Amesema familia hiyo ambayo inajumuisha mke, binti na watoto wawili wa kiume wa Gaddafi waliokimbilia Algeria muda mfupi kabla ya wanamapinduzi kuteka mji wa Tripoli inapaswa kurejeshwa mara moja nchini Libya na kufunguliwa mashtaka mahakamani.
Katika sehemu nyingine ya matamshi yake, Jibril amesema kwamba awali baraza lililotajwa liliazimia kutuma ujumbe wa Libya huko Algeria ili kufuatilia suala hilo lakini kwamba safari hiyo imeakhirishwa baada ya kuuawa Gaddafi. 884201
captcha