Amesisitiza kwamba Marekani ndiyo mpinzani mkubwa wa mapinduzi ya wananchi yanayoendelea katika nchi za Kiarabu kwa sababu inatambua vyema kwamba mapinduzi hayo yatahatarisha maslahi yake haramu katika nchi hizo.
Hayo yamesemwa na Ayatullah Sheikh Isa Qassim, khatibu wa Swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Imam Swadiq (as) katika eneo la ad-Diraz, ambapo amekosoa vikali msimamo wa utawala wa Washington kuhusiana na mapinduzi na harakati za wananchi za kupigania uhuru katika nchi za Kiarabu.
Ayatullah Isa Qassim amewatahadharisha madikteta wanaotawala nchi za Kiarabu dhidi ya kukabiliwa na kifo cha kufedhehesha kama kile kilichompata Gaddafi na kuongeza kuwa kifo hicho kinabainisha wazi kwamba siku itafika ambapo watawala wote dhalimu watawajibika mbele ya mataifa yao. Ameshangazwa na baadhi ya nchi za Kiarabu zinazoyataka mataifa mengine kufanya marekebisho ya kisiasa katika hali ambayo zenyewe zinahitaji kufanya marekebisho hayo.
Kiongozi huyo wa Mashia wa Bahrain ameashiria katika sehemu nyingine ya hotuba yake suala la kuachiliwa huru hivi karibuni mateka wa Palestina na kuongeza kuwa licha ya kuwa wafungwa hao wameachiliwa huru lakini bado kuna mateka wengine wengi wa Kipalestina katika jela za kuogofya za utawala haramu wa Israel, ambao amesema wataachiliwa huru tu kupitia mapambano.
Wakati huohuo ameashiria hali ya wafungwa wa kisiasa wa Bahrain na kusema kuwa hali ya wafungwa hao ambao ni pamoja na wanawake, inaendelea kuwa mbaya siku hadi siku na hii ni katika hali ambayo utawala unaotawala nchi hiyo wa Aal Khalifa unadai kwamba unaheshimu haki za wanawake. 884338