Kwa mujibu wa gazeti la al Yaum as-Sabe' wakaazi wa mji huo ulioko magharibi mwa mkoa wa Luxor wamesema kuwa wamechukizwa mno na hatua ya afisa mmoja wa idara hiyo ya kuvunjia heshima Uislamu na kitabu kitukufu cha Qur'ani.
Katika mvutano uliozuka hivi karibuni kati ya afisa huyo na wahudumu wa msikiti mmoja wa Armant, afisa huyo alitoa maneneo ya kashfa dhidi ya Uislamu na kutupa chini Qur'ani Tukufu.
Baada ya kusikia maneno hayo ya kashfa walioshuhudia na kusikia maneneo hayo ya matusi walichukua hatua ya kumshitaki afisa huyo wa Idara ya Wakfu kwa idara kuu ya mwendesha mashtaka katika mji huo na kutaka afutwe kazi mara moja.
Kuhusu jambo hilo, Sheikh Abdul Adhim al-Qadhi, mkuu wa Idara ya Wakfu ya mji wa Armant amesema kwamba uchunguzi kuhusiana na tukio hilo unaendelea na kwamba malalamiko dhidi ya afisa huyo yatafikishwa katika makao makuu ya Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu mjini Cairo kwa ajili ya kuchukuliwa hatua. 884779