IQNA

Hali ya afya ya dikteta wa Misri yazidi kuzorota

17:44 - October 25, 2011
Habari ID: 2211743
Vyanzo vya kuaminika vya Misri vimetangaza hivi karibuni kwamba hali ya afya ya Hosni Mubarak dikteta aliyeng'olewa madarakani wa Misri inazidi kuwa mbaya.
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, hivi sasa Mubarak anatibiwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi katika Kituo cha Kimataifa cha Tiba nchini Misri. Inasemekana kuwa madaktari wanaomhudumia Mubarak wanafanya kila wawezalo ili kuokoa maisha yake.
Kabla ya hapo baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kuwa Mubarak amepatwa na mshtuko wa ubongo na kupelekea ubongo wake kutofanya kazi tena, jambo ambalo viongozi rasmi wa nchi hiyo wamejiepusha kulithibitisha au kulikadhibisha.
Chombo kimoja cha tiba kimesema kuwa hali ya afya ya Mubarak ilizorota sana mara tu baada ya kushuhudia jinsi dikteta mwenzake wa Libya Kanali Mummar Gaddafi alivyouawa. Kimesema hali hiyo ilimuathiri sana kiasi kwamba alianza kulia kama mwendawazimu. 886453
captcha