IQNA

Ukakamavu wa Iran mbele ya ubeberu wa dunia; wachochea mwamko wa Kiislamu

11:32 - October 30, 2011
Habari ID: 2214190
Ukakamavu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mbele ya ubeberu na siasa za mabavu za madola makubwa ya dunia umewapa moyo Waislamu wa mataifa mengine kuchukua msimamo kama huo na hivyo kuchochea mwamko wa Kiislamu duniani.
Hayo yamesemwa na Abdul Manan Abdul Rahman, mkuu wa gazeti la Muslim News kutoka nchini Ghana. Amesema Iran ni nguzo muhimu ya ulimwengu wa Kiislamu na kwamba ni mfano wa kuigwa na Waislamu wote wawe Mashia au Wasuni.
Amesema Iran daima imekuwa ikisimama imara na bila kuchoka mbele ya ubeberu wa madola ya Magharibi na utawala ghasibu wa Israel na kwamba haijawahi kusita hata kidogo katika kuzisaida jamii na nchi dhaifu za Kiislamu katika kupigania uhuru na haki zao. Amesema ni kutokana na ukweli huo ndipo Iran ikaendelea kuhuisha moyo wa matumaini na matarajio katika nyoyo za Waislamu.
Kuhusu juhudi za maendeleo zinazotekelezwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Ghana Bwana Abdul Raham amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu imejenga chuo kikuu cha pekee cha Kiislamu nchini humo na kwamba ina vituo vingi vya afya na tiba vilivyoanzishwa kwa lengo la kuwasaidia Waislamu wa nchi hiyo.
Abdul Rahman ambaye yuko mjini Tehran kwa lengo la kushiriki katika tamasha la kimataifa la magazeti na mshirika ya habari amesema kwamba gazeti lake la Muslim News licha ya kuakisi habari muhimu za utamaduni, jamii, familia na masuala ya michezo ndilo la pekee linaloandika na kuakisi habari na matukio yanayohusiana na ulimwengu wa Kiislamu nchini humo. 889163
captcha