IQNA

Kongamano la kimataifa la Uchumi wa Kiislamu laanza Malaysia

11:53 - October 30, 2011
Habari ID: 2214210
Kongamano la kimataifa la "Uchumi wa Kiislamu, Wakfu, Zaka na Sadaka, Nyenzo za Kuiwezesha Jamii" lilianza jana katika jimbo la Kedah nchini Malaysia.
Shirika la habari la Malaysia Barnama limeripoti kuwa kongamano hilo la siku tatu linasimamiwa na Kituo cha Kimataifa cha GCIBFE na limefunguliwa kwa hotuba ya waziri mkuu wa zamani nchi hiyo Mahathir Muhammad.
Miongoni ma malengo ya kongamano hilo ni kunyanyua juu kiwango cha uelewa kuhusu uchumi na benki za Kiislamu, kutayarisha mazingira bora ya kubadilishana uzoefu katika nyanja za uchumi na benki za Kiislamu na kufanya juhudi za kuboresha mustakbali wa jamii ya Kiislamu.
Kongamano hilo la kimataifa la Uchumi wa Kiislamu litakamilisha shughuli zake kesho Jumatatu. 889204
captcha