IQNA

Mwana wa Gaddafi apewa himaya na Mawahabi wa Saudia

10:29 - October 31, 2011
Habari ID: 2214878
Mwana wa dikteta wa zamani wa Libya Saadi Gaddafi Jumamosi iliyopita alipelekwa Jiddah Saudi Arabia akitokea Niger na kupewa himaya na Mawahabi wa nchi hiyo.
Gazeti la al Watan la Saudi Arabia limeripoti kuwa Saadi Gaddafi aliwasili nchini humo akifuatana na kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa Saudia.
Gazeti hilo limeripoti kuwa Saadi alipelekwa Saudia na ndege ya Uturuki na kwamba safari hiyo imetayarishwa na Mawahabi wa nchi hiyo.
Ni vyema kukumbusha kuwa Saadi Gaddafi alikimbilia Niger baada ya mji wa Tripoli kutekwa na wanamapinduzi wa Libya na kusambaratika serikali ya baba yake, Muammar Gaddafi. 890052

captcha