Ekmeleddin Ihsanoglu amesema katika taarifa hiyo kwamba mashambulizi ya anga yanayofanywa na jeshi la Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza ni jinai kubwa na ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa. Ameongeza kuwa jinai hiyo inatishia usalama wa eneo zima la Mashariki ya Kati.
Katibu Mkuu wa OIC amesema kuwa utawala ghasibu wa Israel ndio utakaolaumiwa kutokana na athari mbaya za kuwashambulia raia wa Palestina katika Ukanda wa Gaza. Ihsanoglu amelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kamati ya pande nne ya umoja huo kutekeleza wajibu wao na kusimamisha mara moja jinai za Israel huko Palestina.
Wakati huo huo harakati ya Hamas imetangaza kwamba makundi ya mapambano ya ukombozi ya Palestina yatajibu jinai zinazoendelea kufanywa na utawala ghasibu wa Israel huko Palestina. 891368