Kwa mujibu wa tovuti ya saphirnews, sehemu ya kwanza ya filamu hiyo ambayo imegawanywa katika sehemu 8, na ambayo ina lengo la kuarifisha mila na desturi za Waislamu na kuondoa dhana mbaya iliyoko katika jamii ya Wamarekani kuhusiana na Uislamu, itaanza kuonyeshwa tarehe iliyotajwa kupitia televisheni ya TLC.
Filamu hiyo inazungumzia maisha ya kawaida ya familia tano za Kiislamu zikiwa nyumbani kwao na kwenye misikiti. Familia hizo zinaishi katika viunga vya mji wa Detroit katika jimbo la Michigan Marekani.
Waongozaji wa filamu hiyo hawakuuchagua mji huo kisadfa tu bila dalili yoyote, bali ni kutokana na ukweli kuwa mji huo ndio ulio na msikiti mkubwa zaidi kaskazini mwa Marekani. Sababu nyingine ni kuwa Waislamu wamekuwa wakiishi katika mji huo kwa miaka mingi. 891881