IQNA

Waislamu Karbala waandamana kuunga mkono mapinduzi ya Bahrain

21:13 - November 05, 2011
Habari ID: 2217956
Watu wa mji mtakatifu wa Karbala nchini Iraq wameandamana leo wakiunga mkono harakati ya mapinduzi ya wananchi wa Bahrain.
Watu waliokwenda kuzuru Haram ya mjukuu wa Mtume Muhammad (saw) katika mji mtakatifu wa Karbala walijiunga na maandamano hayo wakiwaunga mkono wanamapinduzi wa Bahrain na kulaani jinai zinazoendelea kufanywa na utawala wa Aal Khalifa dhidi ya wananchi.
Maandamano hayo yamefanyika katika eneo lililoko mkabala wa uwanja wa baina ya Haram mbili za Imam Hussein (as) na ndugu yake Abbas bin Ali (as).
Ripoti zinasema kuwa Waislamu walikwenda kuzuru kaburi la Imam Hussein (as) kutoka nchi za Kiarabu walijiunga na maandamano hayo na kutangaza uungaji mkono wao kwa ndugu zao wanaodhulumiwa wa Bahrain. 893501

captcha