Sheikh Hassan Saffar amesema ibada ya Hija inawakutanisha Waislamu kutoka maeneo mbalimbali duniani na mahujaji wanapaswa kuzima njama za maadui wa Uislamu za kuzusha hitilafu na mifarakano kati ya Waislamu kwa kuimarisha umoja na mshikamano.
Amesema ibada ya Hija ni fursa ya Waislamu kuonyesha umoja wao kivitendo na Waislamu wanapaswa kuitumia vizuri fursa hiyo.
Mwanazuoni huyo wa Kiislamu pia amekosoa mwenendo wa serikali ya Saudi Arabia wa kubomoa turathi za Kiislamu na kihistoria katika miji mitakatifu ya Makka na Madina na kuongeza kuwa vitendo hivyo vinawafanya Waislamu wasitambue historia ya dini yao.
894762