Kundi hilo linaloongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Vatican Jean-Louis Tauran, litatembelea pia vituo kadha vya Kiislamu katika mji wa Mumbai huko India.
Ajenda kuu ya safari ya ujumbe wa Vatican ni kujadili njia za kuimarisha mazungumzo kati ya Waislamu na Wakristo, kuzuia mapigano ya kidini na kikaumu na kujadili hali ya Waislamu na Wakristo katika miji mbalimbali ya India.
Ujumbe huo wa Vatican pia utakutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa dini nyinginezo. 894832