IQNA

Jordan yashiriki katika ukandamizaji dhidi ya wananchi wa Bahrain

15:28 - November 09, 2011
Habari ID: 2219608
Mwandishi mmoja wa Kiarabu ameashiria uhusiano mkongwe uliopo kati ya serikali ya Jordan na watawala dhalimu wa Bahrain na kusema kuwa serikali hiyo imekuwa ikishirikiana kwa karibu na utawala wa Manama katika kutesa na kuwakandamiza wanamapinduzi wa Bahrain wanaoshikiliwa katika jela za nchi hiyo.
Hayo yamesemwa na Abdallah Mu'min mwandishi mashuhuri katika ulimwengu wa Kiarabu na kuongeza kuwa kila mwezi wa Disemba utawala wa Manama hutangaza habari zisizo na msingi za kuvunjwa mitandao inayodaiwa kutaka kuuangusha utawala wa ukoo wa Aal Khalifa nchini humo nayo serikali ya Jordan kutuma nchini humo wahanga wa madai hayo ambao huwa tayari wamehojiwa na kuteswa kinyama na serikali hiyo.
Mwandishi huyo mashuhuri amesema kuwa Wabahrain mara kwa mara huzitaka jumuiya na mashirika ya kimataifa kuwaandama na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria vibaraka wa serikali ya Jordan ambao hujihusisha na mateso dhidi ya raia wasio na hatia wa Bahrain.
Abdallah Mu'min amesisitiza kwamba utawala wa Bahrain unawatumia vibaraka hao wa Jordan katika Wizara za Ulinzi na Mambo ya Ndani za Bahrain kukandamiza na kuvunja maandamano halali ya Wabahrain. 895404
captcha