IQNA

Ikhwanul Muslimin:

Hatutaacha kaulimbiu ya 'Uislamu Ndio Suluhisho'

17:59 - November 09, 2011
Habari ID: 2220009
Kiongozi wa ngazi za juu wa chama cha Ikhwanul Muslimin Ali Abdul Fattah amesema kuwa chama hicho hakitatupilia mbali kaulimbiu ya 'Uislamu Ndio Suluhisho'.
Gazeti la al Ahram limeripoti kuwa Ali Abdul Fattah amesema harakati hiyo haitatupilia mbali kaulimbiu hiyo katika kampeni za uchaguzi ujao. Amesema kaulimbiu hiyo ni nara ya kisheria inayobainisha itikadi za Ikhwanul Muslimin na si nara ya kidini pekee.
Amesisitiza kuwa wagombea wengine wa kujitegemea pia wanatumia nara hiyo.
Uchaguzi wa bunge la Misri utafanyika tarehe 27 Novemba. 895553

captcha