IQNA

Wananchi wa Marekani wanataka rais anayezingatia masuala ya kidini

22:04 - November 10, 2011
Habari ID: 2220143
Kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni uliofanyika hivi karibuni nchini Marekani wananchi wa nchi hiyo wanataka kuwa na rais aliye na itikadi madhubuti za kidini.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Kituo cha Utafiti wa kidini mjini Washington, thuluthi mbili ya wananchi hao wanaamini kwamba mgombea kiti cha rais wa nchi hiyo anapasa kuwa na imani thabiti za kidini hata kama imani hizo zitapingana na imani zao wenyewe za kidini.
Kwa mujibu wa matokeo ya uchunguzi huo yaliyotangazwa rasmi siku ya Jumanne, asilimia 67 ya Wamarekani wanapinga vikali kuchukuliwa hatamu za uongozi wa nchi hiyo rais asiyemwamini Mungu.
Matokeo hayo pia yanaonyesha kuwa ukosefu wa ajira ni tatizo kubwa zaidi linalowatatiza Wamarekani na kwamba ndilo litakaloainisha mtu atakayechaguliwa katika uchaguzi ujao wa rais wa nchi hiyo.
Awamu ya 57 ya uchaguzi wa rais wa Marekani imepangwa kufanyika tarehe 7 Novemba mwaka ujao wa 2012. 895616
captcha