Harakati za Ikhanul Muslimin ya Misri na An Nahda ya Tunisia zilikuwa vyama vikuu vya upinzani katika nchi hizo kwa miongo kadhaa na baada ya ushindi wa An Nahda Tunisia, kuna uwezekano mkubwa wa Ikhwanul Muslimin kushinda katika uchaguzi ujao nchini Misri.
Hayo ni kwa mujibu wa Emiliano Mrochi Mtaliano mtaalamu wa masuala ya Mashariki ya Kati katika mahojiano aliyofanyiwa na IQNA.
Amesema wananchi wa Misri wanaunga mkono vyama vya Kiislamu kwa sababu vinaunga mkono sera za demokrasia. Amesema kuwa pamoja na kuwa hakukuwepo vyama nchini Libya, nchi hiyo itashuhudia mwelekeo wa Kiislamu katika katiba mpya.
Amongeza kuwa watu wa Ulaya wanaunga mkono mwamko wa Kiislamu katika nchi za Kiarabu, ingawa serikali za Ulaya zimekuwa zikipendelea kurejea madarakani watawala madikteta waliotimuliwa madarakani.
Mwanadiplomasia huyo wa Italia ametoa wito kwa nchi za Ulaya na Marekani kutoingilia mkondo wa marekebisho katika nchi za Kiarabu. 895761