IQNA

Vipande vya ngurue vyazikwa katika ardhi ya msikiti Uswisi

17:56 - November 14, 2011
Habari ID: 2222722
Katika tukio lililowashtua Waislamu waishio kwa amani Uswisi, watu wenye chuki dhidi ya Uislamu wamezika vipande vya ngurue katika ardhi iliyopangwa kujengwa msikiti.
Abdel Azziz Qasim msemaji wa Baraza Kuu la Kiislamu Uswisi amesema: ‘Tokea wakati ujenzi wa minara ya misikiti ulipopigwa marufuku, kumekuwepo na ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu kwa hivyo tukio kama hili tulilitarajai’.
Vipande vya ngurue vilipatikana vimezikwa katika ardhi iliyopangwa kujengwa msikiti katika mji wa Grenchen nchini Uswisi.
Tukio hilo chafu liligunduliwa Ijumaa wakati polisi walipopokea ujumbe kuwa vipande vya ngurue vimezikwa katika uwanja wa ujenzi wa msikiti.
Waraka huo ulioandikwa kwa lugha ya Kijerumani ulisema: ‘Hii oparesheni inalenga kulalamikia kuenea Uislamu nchini Uswisi’.
Kuna karibu Waislamu nusu milioni kati ya watu milioni 7 nchini Uswisi.
898437
captcha