IQNA

Semina ya ‘Ghadir’ yafanyika India

16:10 - November 16, 2011
Habari ID: 2223390
Kwa munasaba wa sikukuu ya Idd al Ghadir semina ya siku moja ilifanyika Novemba 13 katika Ukumbi wa Almas katika eneo la Hussein Abad huko Lucknow India.
Semina hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya Ghadir Mission kwa ushirikiano na mwakilishi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa ilianza kwa kiraa ya Qur’ani Tukufu na hotuba ya Hujjatul Islam Sayyid Etrat Hussein Razavi ambaye ni mkuu wa taasisi hiyo.
Vile vile akihutubia hafla hiyo Hujjatul Islam Qazvini ambaye ni mwanachama wa Bodi ya Sayansi ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Ahlul Bayt AS aliashiria umuhimu wa tukio la Ghadir na kusema kukubali utawala au wilaya ya Imam Ali AS ni mhimili wa umoja wa Kiislamu.
898503
captcha