Mwanachama wa Kamati ya VIII ya Bunge Adang Ruchiatna amesema bodi hiyo itawajibika moja kwa moja kwa Rais ili kuzuia ufisadi wa aina yoyote ile.
Pendekezo hilo limetangazwa katika fremu ya marekebisho ya sheria ya Hija nchini humo. Bodi hiyo inatazamiwa kuhakikisha kuwa huduma bora za Hija zinatolewa kwa umma. Kati ya mapendekezo mengine ni kuruhusiwa mashirika binafsi ya ndege nchini humo kuwabeba mahujaji hadi Saudia.
Adang amesema gharama ya safari ya Hija ni ghali mno nchini Indonesia ikilinganishwa na nchi zingine za Kusini mashariki mwa Asia. Ametoa mfano wa Malaysia ambapo safari ya Hija kwa mtu moja hugharimu US$ 2500 na Ufilipino ikiwa ni US$1500 katika hali ambayo nchini Indonesia ni US$ 3500.
899554