Rami Abduh ambaye ni mwanachama wa Kamati ya Kimataifa ya Kufuta Mzingiro wa Ghaza amesema kuwa ujumbe huo wa kimataifa utaingia Gaza kwa kaulimbiu ya 'Msimu wa Machipua ya Uhuru' kwa ziara ya siku nne. Amesisitiza kuwa ujumbe huo wa kimataifa kesho utatoa taarifa ya 'Tangazo la Kimataifa la Kupinga Mzingiro dhidi ya Mataifa Mbalimbali'.
Ameongeza kuwa safari ya ujumbe huo imetayarishwa na kampeni ya Ulaya ya kupambana na mzingiro wa utawala ghasibu wa Israel dhidi ya raia wa Ghaza yenye makao yake mjini Brussels, Ubelgiji ikishirikiana na Jumuiya ya Maulamaa wa Kiislamu wa Misri.
Rami Abduh amesema wawakilishi wa zaidi ya nchi 150 hususan kutoka Ulaya na America ya Latini wanashiriki katika ujumbe huo. Amesema msafara mwingine kutoka nchi za Kiafrika utajiunga na ujumbe huo siku mbili baadaye.
Ujumbe huo wa kimataifa utakutana na wanasiasa wa Palestina akiwemo Waziri Mkuu wa serikali halali ya Palestina Ismail Hania na wanaharakati wa Ukanda wa Gaza. 902573