Kongamano hilo linafanyika kwa mwaka wa 8 mfululifo kwa hima ya Taasisi ya Nakala za Maandishi ya Mkono ya Kiislamu ikishirikiana na Jumuiya ya Hazina za Kiislamu na Kituo cha Utafiti wa Kiislamu cha Talal bin Walid cha Chuo Kikuu cha Cambridge.
Kongamano hilo litajadili maudhui kama uchunguzi kuhusu mada zilizotumika katika uandishi wa nuskha za maandishi ya mkono na karatasi zake, utafiti kuhusu nuskha za masuala ya kisayansi, uchunguzi kuhusu nakala za maandishi ya mkono ya wasanii, faharasa za nuskha za maandishi ya mkono ya Kiislamu na kadhalika.
Makala 25 za kielimu zitawasilishwa pia katika kongamano hilo la kimataifa. 902286