Akizungumza Novemba 21 katika hafla ya wahadhiri na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Ulinzi nchini Iran, Dkt Mohammad Baqer Khorramshadi ameongeza kuwa, Marekani kila siku inapanga njama za kuishinikiza na kuitenga Iran lakini situ kuwa njama hizo hazijafua dafu lakini nchi za kieneo zinakurubiana zaidi na Iran.
Ameashiria mapinduzi mbalimbali ambayo yamewahi kujiri duniani na kusema mapinduzi ya sasa katika eneo la Mashariki na Kati na kaskazini mwa Afrika yanashabihiana kwa baadhi ya nukta na Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na ndio sababu watu wengi wa nchi za maeneo hayo wamejitokeza katika medani za mwamko na kudhihirisha chuki yao dhidi ya utawala wa Kizayuni na mabeberu.
Dkt. Khorramshad amesema mpango wa ‘Mashariki ya Kati Kuu’ uliopendekezwa na rais wa zamani wa Marekani George W. Bush ulikuwa njama iliyofeli ya kujaribu kuzima mwamko wa Kiislamu.
903713